
Akiwa amewasili Niger siku moja kabla, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, amezuru eneo la uchimbaji madini la Somaïr huko Arlit, kaskazini mwa nchi hiyo, siku ya Jumatano, Machi 12, ambapo zaidi ya tani 1,400 za madini ya uranium zimehifadhiwa tangu Niamey kuzuia mauzo yake nje.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Miezi mitano baada ya ziara ya mwisho ya mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) nchini Niger – mwezi Oktoba – Niamey ilimpokea, siku ya Jumanne, Machi 11, mkurugenzi wake mkuu, Rafael Grossi, ambaye hajawahi kuzuru nchi hiyo tangu aingie madarakani miaka mitano iliyopita.
“IAEA iko tayari kuunga mkono Niger katika afya, nishati na mazingira, kupitia sayansi na teknolojia ya nyuklia,” shirika hilo limeandika katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X ambapo pia limemshukuru Waziri wa Nishati wa Niger, Haoua Amadou, kwa mapokezi yake mazuri.
Kama moja ya dhamira kuu za IAEA ni kuhakikisha usalama na matumizi ya vifaa vya mionzi, kwa hiyo Rafael Grossi amezuru Arlit, mgodi wa uranium wa Somaïr, kampuni tanzu ya mwisho ya Orano nchini Niger, ambayo bado inafanya kazi, ambapo kampuni ya Ufaransa inasema imepoteza udhibiti wa utendaji kufuatia mzozo na serikali ya Niger, mbia mwenza, ambayo pia ilifunga mpaka wake na Benin, eneo ambapo mafuta ya nyuklia yalikuwa yakisafirishwa nje ya nchi. Kama matokeo, hifadhi kwenye eneo hilo inaongezeka, na takwimu ya zaidi ya tani 1,400 za mkusanyiko wa uranium iliyohifadhiwa kwenye eneo hilo inawekwa kwa sasa.
Wakati mamlaka ya Niger tayari imetaja ushirikiano mpya na Urusi, Uturuki au Iran kwa kuiuza, hakuna shaka kwamba suala hilo lilikuwa kiini cha majadiliano.