Uongozi wa kijeshi nchini Niger, umewaachia huru karibu 50, wakiwemo waliokuwa Mawaziri katika serikali ya kiraia iliondolewa madarakani Julai mwaka 2023.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii imekuja kutokana na maazimio yaliyofanyika wakati wa mazungumzo ya kitaifa mwezi Februari.
Mbali na Waziri wa zamani, wengine waliochiwa huru ni pamoja na mwanadiplomasia, mwanahabari na wanajeshi kadhaa waliokuwa wamefungwa jela, kwa tuhma za kupanga mainduzi mwaka 2010.
Aliyekuwa Waziri wa mafuta Mahamane Sani Issoufou, ambaye ni mtoto wa rais wa zamani Mahamadou Issoufou, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Kalla Moutari, na Ahmat Jidoud, aliyekuwa Waziri wa fedha ni miongoni mwa watu mashuhuri walioachiwa huru.

Hata hivyo, aliyekuwa rais Mohamed Bazoum, aliyeondolewa madarakani na jeshi mwaka 2023 hakuwa miongoni mwa watu hao walioachiwa, licha ya shinikizo za kimataifa.
Haya yanajiri, karibu wiki moja baada ya kuapishwa kwa Jenerali Abdourahamane Tiani kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha mpito cha miaka mitano, kama ilivyopendekezwa kwenye mazungumzo ya kitaifa.