Niger :Jenerali Abdourahamane Tchiani ameapishwa kuongoza kwa miaka mitano

Kiongozi wa kijeshi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, ameapishwa siku ya Jumatano, kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha mpito cha miaka mitano.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Tchiani, ameapishwa kuongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi, na kusaini mkataba mpya wa uongozi, unaobadilisha katiba ya nchi hiyo.

Hatua hii, inafuta jitihada za kikanda, ambazo zimekuwa zikiendelea kujaribi kurejesha uongozi wa kiraia, nchini Niger, baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2023.

Mahamane Roufai, Katibu Mkuu wa serikali, akizungumza jijini Niamey, amesema mkataba huo, unaanza kutekelezwa siku ya Jumatano, na umetokana na majadiliano ya kitaifa yaliyopendekeza Jenerali Tchiani, kuongoza kwa kipindi cha mpito cha miaka mitano.

Kipindi hicho cha mpito kinatarajiwa kumalizika mwaka 2030 chini ya ungozi wa Tchiani, ambaye atakuwa ameongoza nchi hiyo kwa jumla ya miaka saba.

Hapo awali, jeshi nchini Niger lilikuwa limeahidi kurejesha madaraka baada ya miaka mitatu, baada ya kuchukua madaraka mwaka 2023 na kuongezwa kwa muda wa mpito, kunafuata nyayo ya mataifa mengine kama Mali, Guinea na Burkina Faso ambayo pia yanaongozwa na wakuu wa majeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *