
Nchini Niger, wasiwasi unaongezeka huko Makalondi, mji wa Tillabéry, katika eneo la Torodi, karibu kilomita 100 kusini magharibi mwa Niamey, karibu na mpaka na Burkina Faso. Kwa wiki kadhaa, wakazi wa Makalondi wamekuwa wakionya kuhusu shinikizo kutoka kwa makundi yenye silaha. Na usiku wa Aprili 6kuamkia Arili 7, kitongoji cha mji huo kilikumbwa na shambulio ambalo halikusababisha hasara yoyote, lakini lilisababisha uharibifu wa mali.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Majivu na mioto michache ambayo bado inaendelea kuwaka inaweza kuonekana kwenye picha zinazoshirikiwa na watumiaji wa mtandao: picha zilizopigwa mapema wiki hii huko Makalondi, takriban kilomita 100 kutoka Niamey, mji mkuu wa Niger. Kulingana na taarifa kutoka kwa vikosi vya ulinzi na usalama iliyorushwa kwenye televisheni ya taifa, karibu maduka ishirini yalichomwa moto wakati wa shambulio lililotekelezwa na kundi lenye silaha usiku wa Jumapili 6 kuamkia Jumatatu Aprili 7.
Shambulio hilo lililenga wilaya ya mji na kituo maalum cha polisi, bila kusababisha hasara yoyote. Uharibifu wa mitambo ya umeme ulisababisha kukatika kwa umeme. Kulingana na vyanzo vya ndani, wakaazi wengine walikimbia shambulio hilo kuelekea Torodi, kaskazini kidogo, au Niamey, ingawa ni vigumu kujua idadi yao.
Hili sio shambulio la kwanza la aina hii. Kwa wiki kadhaa, watu kutoka Makalondi wamekuwa wakishiriki hofu yao kwenye mitandao ya kijamii na kuomba CNSP kuingilia kati kutokana na shinikizo kutoka kwa watu wenye silaha. Katika taarifa yao, vyombo vya ulinzi na usalama vimeeleza kuwa wameimarisha uwepo wao jijini humo na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao.