Netanyahu azuru Hungary, akaidi waranti wa kukamatwa wa ICC

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amewasili Hungary siku ya Alhamisi, na kukaidi waranti wa kukamatwa uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa mwaliko wa mshirika wake mkubwa Viktor Orban.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

“Karibu Budapest!” ameandika Waziri wa Ulinzi Kristof Szalay-Bobrovniczky kwenye Facebook, ambaye alikuja kumsalimia kiongozi huyo kwenye lami ya uwanja wa ndege wa Budapest jana usiku.

Anaanza ziara ya siku nyingi, ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu kuanza kwa vita huko Gaza mnamo mwezi Oktoba 2023. Baada ya heshima za kijeshi katika ikulu ya rais, Bwana Netanyahu atapokelewa asubuhi na mwenzake kwa ajili ya majadiliano na kisha mkutano na waandishi wa habari karibu saa 6:30 mchana saa za Hungary.

Hii ni fursa ya kuhamasisha uungaji mkono wa Hungary kwa mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuudhibiti Ukanda wa Gaza na kuwafukuza wakaazi wake.

Hata hivyo, ziara  hii ni ya kiishara.

Kufuatia tangazo la ICC mnamo mwezi wa Novemba 2024 la hati ya kukamatwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Ukanda wa Gaza, Benjamin Netanyahu amezuru Marekani, lakini hajawahi hajawahi kuzuru nchi yoyote iliyosaini mkataba ya kuundwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.

“Lengo lake kuu ni kurejesha uwezo wa kusafiri popote anapotaka,” Moshe Klughaft, mchanganuzi na mshauri wa zamani wa kiongozi huyo wa Israeli, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kupitia ziara hii “katika nchi ambayo haogopi kukamatwa, anafungua njia ya kuhalalisha ziara yake ya baadaye,” labda kwa mfano hadi Ujerumani, ambapo Kansela wa baadaye Friedrich Merz amehakikisha kwamba angeweza kuja bila kuwa na wasiwasi.

– “Wajibu wa Kisheria” – 

Viktor Orban alimwalika mara tu habari za ICC zilipojulikana, akisema “alishtushwa na uamuzi wa aibu.” Kwa upande wake, Bw. Netanyahu amesifu “uwazi wa kimaadili” wa Hungary.

Ikiwasiliana na AFP, mahakama imekariri “wajibu wa kisheria” wa Budapest na “wajibu wake kwa nchi zingine” kutekeleza maamuzi.

“Ikiwa mataifa haya yana wasiwasi kuhusu ushirikiano wao na Mahakama, yanaweza kushauriana nayo,” amebainisha msemaji wake, Fadi El Abdallah. “Lakini si juu yao kuamua kwa upande mmoja ubora wa maamuzi ya kisheria ya ICC.”

Nchi hiyo ya Ulaya ya Kati inataka kufika mbali zaidi na inatarajiwa kutangaza kujiondoa katika Mahakama hiyo, kwa mujibu wa ripoti kutoka Radio Free Europe, zikinukuu vyanzo vya kidiplomasia.

Hungary ilitia saini Mkataba wa Roma, mkataba wa kuanzilishwa kwa ICC, mwaka 1999, na kuuidhinisha miaka miwili baadaye, wakati wa muhula wa kwanza wa Viktor Orban.

Lakini haikuidhinisha mkataba husika kwa sababu za kikatiba na hivyo inadai kutolazimika kuzingatia maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa.

– Msukosuko wa ndani – 

Mahakama hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2002, sasa ina wanachama 125 na ina jukumu la kushtaki uhalifu mkubwa zaidi duniani wakati nchi hazitaki au haziwezi kufanya hivyo zenyewe. Hadi sasa, ni nchi mbili pekee ambazo zimejitenga na mahakama hiyo: Burundi na Ufilipino.

Wakati serikali ya Hungary inaibua mara kwa mara wazo la kujitoa katika taasisi inayoiita kuwa “inayoegemea,” kwa hiyo itakuwa tayari kuchukua hatua hiyo, ikifuata nyayo za Donald Trump, ambaye aliiwekea vikwazo Mahakama ya ICC mwezi Februari kwa kile alichoeleza kuwa “vitendo haramu na visivyo na msingi vinavyolenga Marekani na mshirika wetu wa karibu Israeli.”

Benjamin Netanyahu anaondoka Jerusalem wakati kunaripotiwa msukosuko mkubwa wa ndani huku akiwa katika mzozo na Mahakama ya Juu, ambayo imezuia uamuzi wa serikali wa kumfukuza kazi mkuu wa sasa wa Shin Bet.

Aidha, washauri wake wawili kwa sasa wako chini ya ulinzi katika kesi iliyopewa jina la “Qatargate” na vyombo vya habari vya Israeli. Wanashukiwa kupokea fedha kutoka Qatar ili kukuza maslahi ya Israeli ya Ghuba Imarati, mwenyeji wa viongozi wa Hamas na mpatanishi kati ya Israelina vuguvugu hili la Kiislamu la Palestina.

Netanyahu atareje nchini siku ya Jumapili, kulingana na Bw. Klughaft.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *