Netanyahu ataishia kwamba Israel itachukua baadhi ya maeneo ya Gaza

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihotubia bunge, ametishia kuwa jeshi la nchi hiyo, litalazimika kuchukua baadhi ya maeneo ya Gaza, iwapo kundi la Hamas, halitawaachia huru mateka wote wanaoendelea kushikiliwa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Aidha, Netanyahu amewashtumu wanasiasa wa upinzani kwa kuchochea machafuko nchini umo kwa kufadhili maandamano dhidi ya serikali, kama ilivyoshuhudiwa katika siku zilizopita.

Maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakijitokeza jijini Jerusalem, kumshtumu Netanyahu kwa kutoheshimu hali ya kidemokrasia nchini humo na kuanza tena mashambulio ya angaa kwenye ukanda wa Gaza, bila kuwajali mateka.

Israel inaituhumu Hamas kwa kutowaachia mateka wote
Israel inaituhumu Hamas kwa kutowaachia mateka wote © Abdel Kareem Hana / AP

Wakati hayo yakijiri, Wapalestina karibu 40 wameuawa kwenye ukanda wa Gaza, baada ya kushambuliwa na wanajeshi wa Israeli, kwa mujibu wa Wizara ya afya kwenye ukanda huo.

Kundi la Hamas nalo limeonya kuwa iwapo Israel itaendeleza mashambulio yake, au kujaribu kuwaokoa mateka kwa nguvu, watarejeshwa wakiwa kwenye majeneza.

Nayo Tume ya Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia masuala ya kibinadamu OCHA, imesema Wapalestina wapatao 142,000 wamelazimika kuyakimbia makaazi yao, baada ya Israeli kuanza mashambulio mapya Machi 18.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *