Netanyahu ajificha kwenye ‘chumba cha chini ya ardhi’ kwa kuhofia mapigo ya Wanamuqawama

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameripotiwa kuwa anafanya kazi kutoka kwenye “chumba cha chini ya ardhi” kwa hofu ya ulipizaji kisasi na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na harakati za Muqawama wa Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi.

Chinja chinja huyo wa watu wa Gaza amekuwa akiandaa “mikutano ya kiusalama” ya utawala huo katika chumba hicho cha chini ya ardhi katika mji mtakatifu wa Quds Tukufu unaokaliwa kwa mabavu na Israel huku kukiwa na hatua kali za ulinzi.

Netanyahu amekuwa akitumia eneo hilo tangu Oktoba, wakati ndege isiyo na rubani ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon iliposhambulia makazi yake katika mji wa Caesarea, kaskazini mwa Tel Aviv.

Haya yanajiri baada ya mifumo ya makombora ya utawala huo dhalimu kushindwa kuzuia ndege hiyo isiyo na rubani, na baada ya kile kinachojulikana kama “Kamanda wa Mbele ya Nyumbani” kushinda kutoa tahadhari yoyote.

Mnamo Agosti, ndege isiyo na rubani ya Hizbullah ya Lebanon  ilipenya katika sehemu ya kaskazini ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, na kupiga picha kwenye makazi hayo.

Mwishoni mwa Septemba pia, Vikosi vya Jeshi la Yemen lilitangaza kuwa limelenga uwanja wa ndege wa Ben Gurion katikati ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, sanjari na kuwasili huko Benjamin Netanyahu akitokea New York.