‘Nelson Mandela Mwarabu’ aachiwa huru baada ya kufungwa jela miaka 40 nchini Ufaransa

Mahakama ya Ufaransa imeamuru kuachiliwa kwa mwanamapambano wa Lebanon, Georges Ibrahim Abdallah, ambaye alikamatwa miaka 40 iliyopita kutokana na mauaji ya maajenti wa Marekani na Israel mjini Paris.

Abdallah anayejulikana kwa jina la “Nelson Mandela wa Ulimwengu wa Kiarabu” aliwekwa kizuizini mwaka 1982 na alikuwa mfungwa aliyekaa muda mrefu zaidi gerezani Ulaya Magharibi. Amefungwa nchini Ufaransa kutokana na uamuzi wa kisiasa wa mfumo wa mahakama wa nchi hiyo, ambao umeidhinisha kuachiliwa kwake mara tatu.

Mahakama hiyo imekubali Georges Ibrahim Abdallah achiliwe huru kuanzia Desemba 6, kwa masharti kwamba aondoke nchini Ufaransa na asidhihiri tena nchini humo.

Abdallah alikuwa mwanachama wa zamani wa Front for the Liberation of Palestine (PFLP) na kundi la Armed Revolutionary Factions (LARF).

Mnamo 1982 kundi la mapambano la Abdallah, LARF, lilikifri kuhusika na mauaji ya mawakala wa Israel na Marekani huko Paris.

Georges Ibrahim Abdallah alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 1987 baada ya kushtakiwa kwa mauaji ya mwambata wa kijeshi wa Marekani, Charles Ray na mwanadiplomasia wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Yakov Barsimentov mjini Paris.

Kesi ya Abdallah ilijulikana kwa kukosa ushahidi wa kuthibitisha tuhuma zilizomkabili, na wakili wake mwenyewe baadaye alikiri kwamba alikkuwa akifanya kazi kwa siri serikalini.