Ndoa ya kisiasa ya Raila na Ruto itabadili vipi siaza za Kenya?

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, sio mgeni katika mchezo wa karata za kisiasa za ndani na nje ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Katika miaka zaidi ya arobaini ambayo amekuwa akipiga siasa zake ndani ya Kenya, hajakosa kufanya maamuzi ya kisiasa yaliyowaacha wengi vinywa wazi.