Ndege ya Ukraine F-16 yadunguliwa katika shambulizi la Urusi – BBC

Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameitaka Ulaya
kusaidia kukabiliana na tishio la usalama linaloongezeka huko Sahel, eneo tete
ambalo limekabiliwa na mfululizo wa mashambulizi mabaya katika siku chache
zilizopita.

Ametoa wito huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
akiwa na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, ambaye alikuwa anamaliza ziara
yake Afrika Magharibi.

“Hali katika eneo la Sahel inataka uhamasishaji wa
kimataifa wa jumuiya ya kimataifa,” alisema Rais Faye, ambaye pia
anahudumu kama mwezeshaji katika juhudi za ECOWAS kurejesha Mali, Niger, na
Burkina Faso katika umoja huo. Alisisitiza haja ya Ulaya kuzidisha uungaji
mkono wake kwa Sahel, ikizingatiwa kwamba “Afrika na Ulaya zina hatima
iliyounganishwa ya usalama.”

Ombi lake linawadia siku chache baada ya Burkina Faso
kushuhudia moja ya mashambulizi yake mabaya zaidi.

Makumi ya raia na vikosi vya usalama waliuawa na
wanamgambo katika eneo la Kaskazini la Barsalogho mnamo Agosti 24.

Kundi la wanajihadi lenye uhusiano na Al-Qaeda, Jama’at
Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) lilidai kuhusika na shambulio hilo la
kikatili, ripoti zikidokeza kuwa watu 200 waliuawa kwa jumla wakati wakichimba
mitaro ili kulinda kijiji chao dhidi ya wanamgambo.

Mamlaka za Burkina Faso, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
EU, Marekani na hata ECOWAS walilaani shambulio hilo.

Bado haifahamiki jinsi Burkina Faso, Mali, na Niger
zitatafsiri wito wa kiongozi wa Senegal wa kuingilia kati kwa Ulaya katika
mgogoro wa Sahel, kwani walivunja uhusiano na vikosi vya Magharibi na kuwaamuru
watoke katika eneo hilo hilo la Sahel wakati bado hali ikiwa tete.

Nchi hizo tatu ziliunda muungano wa kijeshi ili
kukabiliana na uasi na kuendelea kuwa na uhusisano wa kiusalama na Urusi ambayo
huwapa silaha na wale inaowaita kama “wakufunzi wa kijeshi.”

Soma zaidi: