Ndege ya abiria ya Shirika la Air India AI 171 iliyokuwa ikielekea London, imepata ajali katika eneo la makazi karibu na Uwanja wa ndege wa Ahmedabad, maafisa wa usafiri wa anga wamethibitisha leo.
Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Juni 12, 2025 na ilikuwa na jumla ya watu 242 ndani.
Mamlaka za usafiri wa anga za India zinaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo ambayo shirika la ndege la Air India limeitaja kama “ajali ya kusikitisha.” Vikosi vya uokoaji vilifika haraka eneo la tukio, na shughuli za uokoaji zinaendelea.
Hakuna taarifa rasmi bado kuhusu waliopoteza maisha au walionusurika, lakini ajali hii imezua hofu kubwa kwa familia na jamii ndani na nje ya India.
✍ @claud_jm
📸 @afpphoto
#AzamTVUpdates