Dar es Salaam. Alphard ‘brandi nyuu’. Hapo hamna hamna basi uwe na ‘twente’ milioni. Ili kumiliki mkoko huu wa vinasaba vya kifamilia. Bosi la ‘Dabiliu Sibii Beibi’, Simba la Masimba, Mondi Bin Laden. Katoa ‘frii’ kama zawadi kwa baunsa wake.
Hii ni ‘levo’ ya juu sana ya upendo na kuthamini wanaokuzunguka. Ni ‘levo’ ya juu ya akili ya kutambua na kuelewa umuhimu wa mtu kwenye maisha yako. Hii ni ‘levo’ ya juu mno ya moyo mweupe wa kutoa kwa wengine.
Kabla hujachukulia poa, kama una ndugu mwenye nafuu ya kimaisha. Hebu jiulize mambo uliyomfanyia, yeye alikulipa nini? Kutoa gari siyo kitu kidogo kabisa. Tena kwa mtu ambaye ni mlinzi tu asiyeingiza kitu.

Unaweza kutoa ndinga kwa msanii wako anayekuingizia pesa. Siyo kwa mlinzi ambaye kazi yake ni kukulinda tu. Wenye roho za choyo na kutojua umuhimu wa mtu katika maisha yao hawafanyi alilofanya Mondi.
Hii ni ‘levo’ ya juu kabisa ya uwezo wa kipesa. Siyo kwa mwanamuziki tu hata kwa yeyote. Tunafahamu wana kibao tu ‘wameplei fea’ kwa mabosi wengi mjini hapa. Lakini hawajawahi kupewa ‘jifti’ ya hivi.
Achana na ‘stafu’ wengine kwenye biashara zake. Ambao mara kibao kawapa mikoko. Ninayemuongelea hapa ni ‘baunsa’ mlinzi wa Mondi. Kama ujuavyo waswahili walinzi tunawaona daraja la chini la watu.
Mondi hana mtazamo wa kipimbi. Anajua thamani ya Onesmo, of’kozi na Onesmo anathamini jukumu lake alilopewa. Anajua kazi yake hata video na ‘klipu’ mitandaoni ni ushahidi tosha. Tunamuona mchizi.
Anaweza kuwa kawapa watu wake wengi magari. Lakini zawadi ya gari kwa huyu baunsa wake ina maana pana kuliko mengine. Diamond anatafsiri biashara ya muziki kwa kuiishi.
Diamond anawajibu wazee kibao waliokuwa wanazingua wakati ule. Waliotaka tuamini muziki ni uhuni na kitu cha kupigwa vita. Diamond anaiumbua jamii yenye fikra mbovu kwa miaka na miaka juu ya muziki. Ndiyo!
Enesmo (Baunsa wa Mondi) huyo ni sehemu ya kundi kubwa nyuma ya Diamond. Ambao wanaishi na kuendesha shughuli kifamilia zao kupitia Mondi. Siyo wasanii tu ni wengi wanaokula ‘gud’taim’ kwa sababu yake.
Lakini kwa mtazamo wa fasta fasta ni ngumu. Hata Onesmo pia anajua, kuwa ilikuwa ngumu kuamini kuna siku atapewa ndinga na Diamond. Uchapakazi na uaminifu ndicho kitu pekee kilichofanya apewe ndinga.
Kazi ya ulinzi pamoja na mengine, uaminifu ni kitu cha msingi. Baunsa kibao wamepita kwake na kusepa, ni wazi huyu amekuwa mwema na mwaminifu zaidi kwa ‘big bosi’. Pia na usiri umechangia.
Na hapa ndipo tunarudi miaka 20 nyuma. Pale Water Front jirani na bandari. 2004 kuna Kongamano lilijulikana kama Hip Hop Summit. Lilifanyika na kukusanya wasanii, wadau na wahahidhiri wa kutosha.
Kauli mbiu ya kongamano ilikuwa ni ‘Muziki ni Ajira’. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ndiye aliyeandaa kongamano lile na wadau kadhaa. Marehemu Gardner G Habash ndiye aliyekuwa mshereheshaji siku hiyo.
Wahadhiri kadhaa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walitoa mada na elimu ya kutosha. Lakini majibu ya elimu ile yanakuja kutolewa kwa vitendo na Diamond. Kuwa muziki ni zaidi ya kushika maiki.
Elimu iliyotolewa pale ni pamoja na kukumbusha vijana. Kwamba shule ni muhimu hata kama wanapenda muziki. Muziki unawahitaji wasomi wengi hivyo wakazane na masomo badala ya kukimbilia studio tu.
Juzi kati hapo Mondi alitoa nyumba kwa kaka yake Ricardo. Ilikuwa ni zawadi baada ya kufunga ndoa na akamwambia akaonane na wakili wake wamalize. Siyo akaonane na mjomba sijui mama, hapana Wakili wake.
Kumbe Mondi ili shughuli zake za muziki ziende anahitaji wakili. Pia anahitaji dereva, mtu wa masoko. Achana na meneja, dijei, dansa au prodyuza. Mondi anahitaji wasomi kibao hata mtu wa kumvalisha kila siku (‘stailishi’).
Kumbe msanii mmoja tu anaweza kuzalisha ajira za watu 10 na zaidi. Weka mbali wale wa vibarua vya siku moja moja, hasa kwa zile shoo zake. Hapa tunaoongelea ni wale wa kila siku kwenye maisha yake.
Mondi anahitaji mpishi na daktari. Kaa hiyo usiipoweza kushika maiki utashika kalamu. Unaweza kuwa mwanasheria wao. Meneja wao wa biashara na masoko kuna kazi nyingi ndani ya muziki bila kushika maiki.
Afande Sele alisema… “Siyo lazima wote tuimbee… Onesmo ‘anapushi’ dude kali kuliko wasanii kibao. Ana maisha mazuri kwa pesa za muziki bila kushika miaki wala kudensi. Na ndiyo maana ya muziki ni ajira, kile tulichoambiwa miaka 20 iliyopita.
Simba la Masimba Dangote. Salute!