Nchi zingine 25 za Afrika zaongezwa kwenye orodha ya nchi zilizopigwa marufuku kuingia Marekani

Washington inataka kupanua orodha ya marufuku ya kusafiri kwenda Marekani. Serikali ya Marekani inaripotiwa kufikiria kuweka vikwazo vya usafiri au marufuku kabisa ya kuingia kwa raia wa nchi 36, zikiwemo 25 kutoka bara la Afrika. Washington inataka nchi hizi zitimize baadhi ya masharti ya usalama. Zina siku 60 za kuwa zimetimiza masharti hayo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Atlanta, Edward Maille

Nchi 36 zitakabiliwa na marufuku hiyo, zikiwemo nchi 25 za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Côte d’Ivoire, Gambia, Niger, na Senegal, kulingana na memo ya ndani ambayo Gazeti la Washington Post limepata kopi na baadaye na shirika la habari la Reuters. Hati hiyo iliyotiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, ilitumwa siku ya Jumamosi, Juni 14, 2025, kwa wanadiplomasia kutoka nchi husika. Nchi hizo zina siku 60 kutimiza baadhi ya masharti.

Utawala wa Trump unazingatia kuzuia kuingia kwa raia wa nchi zingine 36a, katika kile ambacho kitakuwa upanuzi mkubwa wa marufuku ya kusafiri iliyotangazwa mapema mwezi huu, kulingana na memo ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Kama uhalalishaji, Washington inaonyesha kuwa baadhi ya nchi haziwezi kutoa “hati za kitambulisho za kuaminika” au kuwa na “udanganyifu wa kupindukia katika utawala.” Kwa nchi zingine, idadi kubwa ya raia wao nchini Marekani “muda wa visa vyao kuishi Marekani ulikwisha kitambo.”

Hatua hii inakuja pamoja na vikwazo vya kuingia vilivyowekwa mapema mwei Juni kwa nchi kumi na mbili, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kongo, Chad, na Haiti, pamoja na vikwazo kwa nchi nyingine kama vile Togo na Burundi. Donald Trump alihalalisha hatua hizi kwa misingi ya usalama wa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *