Nchi za Kiislamu zichukue hatua dhidi ya askari wa Israel aliyevunjia heshima Qur’ani

Kitendo cha hivi punde zaidi cha kuvunjiwa heshima Qur’ani na askari wa utawala haramu wa Israel huko Gaza kimelaaniwa na watu wengi, ikiwa ni pamoja na kundi kubwa zaidi la kutetea Waislamu nchini Marekani ambalo lilitaka Waislamu wachukuliwe hatua dhidi ya hatua hizo za kusikitisha.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR) siku ya Jumanne lililaani kitendo cha mwanajeshi wa Israel cha kuvunjia heshima nakala ya Qur’ani kama kitendo cha hivi karibuni kabisa cha utawala wa Israel katika vita dhidi ya Uislamu na kuyataka mataifa yenye Waislamu wengi kuchukua hatua madhubuti kukomesha utawala huo ghasibu. mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.

Mwanajeshi wa Kiisraeli kutoka Kikosi cha Givati ​​Brigade 435 Rotem aliripotiwa kuchapisha picha yake akikojolea nakala ya Qur’ani Tukufu huko Jabalia, Gaza.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa wa CAIR Nihad Awad alisema:

Serikali ya mrengo mkali wa kulia ya Israel imekuwa ikiendesha vita waziwazi dhidi ya sio tu watu wa Palestina huko Gaza, lakini vita dhidi ya Uislamu na Ukristo. Tangu kuharibiwa kwa misikiti na makanisa, unyanyasaji na udhalilishaji wa wanawake wa Kiislamu, hadi sasa kukojolea nakala za Qur’ani Tukufu, utawala wa Israel umekiuka kila utakatifu ambao Waislamu wanauheshimu.

Jeshi la Israel kwa sasa ni mojawapo ya vikosi visivyo na maadili duniani, na kwa bahati mbaya utawala wa Biden unasalia kuhusika kikamilifu na uhalifu wake wa kivita.

Tunatoa wito kwa mataifa yenye Waislamu wengi kutumia nguvu zao za pamoja, ikiwa ni pamoja na ushawishi wao wa kiuchumi, na kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na serikali hii isiyo na udhibiti na kukomesha mauaji yake ya kimbari.”