
Burkina Faso, Mali na Niger zimeamua kuanzisha ushuru wa forodha wa pamoja wa 0.5% kwa bidhaa wanazoagiza kutoka nchi zilizo nje ya shirikisho lao ili kufadhili shughuli zao. Inayoitwa “tozo ya shirikisho la AES”, hii haipaswi, hata hivyo, kuathiri bidhaa kutoka nchi za WAEMU, ambazo Ouagadougou, Bamako na Niamey bado ni wanachama, ingawa zlijiondoa katika ECOWAS mnamo mwezi wa Januari.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Hati hiyo ambayo imetiwa saini na Assimi Goïta, mkuu wa utawala wa kijeshi huko Bamako ambaye pia anashikilia urais wa zamu wa Muungano wa Nchi za Sahel (AES), inayoanzisha ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoingizwa nchini Mali, Niger na Burkina Faso inatoa utekelezaji wa “tozo ya shirikisho” ya 0.5% kwa bidhaa zinazoingia katika nchi tatu wanachama wa shirika hilo.
Hata hivyo, ushuru huu mpya hautatumika kwa bidhaa zinazosafirishwa au zinazotoka katika nchi za AES, wala hata zile zinazotoka katika taifa lililotia saini nao mkataba wa forodha, nakala inabainisha. Kinadharia, bidhaa kutoka kwa wanachama wa Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (UEMOA), unaojumuisha Mali, Niger na Burkina Faso licha ya kujiondoa kutoka ECOWAS mwezi wa Januari mwaka huu, hazihusiki.
Kwa kweli, ushuru huu utachukua fomu ya uhamishaji wa ushuru wa forodha wa kiwango sawa ambacho tayari kinatumika katika mipaka ya nje ya ECOWAS. Badala ya kuirejesha kwa shirika la kikanda la Afrika Magharibi, nchi za AES zitaiweka ili kuendesha shirikisho lao. Waziri wa Uchumi wa Mali pia ametaka kuwahakikishia wakazi wake: “Kwa watumiaji wa Mali, ushuru huu hauna madhara hata kidogo kwa gharama ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje,” amesema. Hata hivyo, hakuna maelezo yaliyotolewa kwa bidhaa kutoka Ghana na Nigeria, ambazo si wanachama wa WAEMU.