Nchi maskini zaitaka Uingereza kusamehe baadhi ya madini

Wanadiplomasia kutoka nchi nane za kusini na mashariki mwa Afrika wametia saini barua ya kuitaka serikali ya Uingereza kuunga mkono mswada wa kibinafsi unaolenga kuharakisha urekebishaji wa madeni, baada ya mzozo wa kiuchumi kusababisha nchi kushindwa kulipa mikopo yao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Mswada wa Uingereza, uliwasilishwa Novemba 2024 na mbunge wa chama cha Labour, Bambos Charalambous, utazuia wakopeshaji wa kibinafsi kushtaki nchi walizozikopesha wakati mazungumzo ya kufuta madeni yakifanyika.

Nchi ambazo haziwezi tena kumudu kulipa madeni yao zinapaswa kujadiliana na wakopeshaji kuandika barua au kuongeza muda wa mkopo ikiwa ni pamoja na benki za maendeleo zinazomilikiwa na serikali kutoka China, Marekani na Ulaya, katika mchakato unaojulikana kama urekebishaji wa deni.

Tangu mwaka 2020, nchi kadha wa kadhaa zikiwemo Zambia, Sri Lanka na Ghana zimeshindwa kulipa madeni yao ya kigeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *