NBC: Trump amtaka Zelensky ampatie umiliki wa asilimia 50 wa madini adimu ya Ukraine

Kwa mujibu wa maafisa wanne wa Marekani, utawala wa Trump umependekeza kwa Ukraine kwamba iwapo nchi hiyo itaipatia Marekani asilimia 50 ya madini yake adimu, iko tayari kutuma wanajeshi wake ili kuilinda Ukraine iwapo itafikia makubaliano na Russia.