
Rais Donald Trump siku ya mnamo Alhamisi, Machi 6, kwa mara nyingine tena ametilia shaka kujitolea kwa Marekani kwa NATO, akisema kwamba Marekani haipaswi kusaidia nchi ambazo, machoni pake, hazitumii vya kutosha kujilinda.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Washington kwamba hatozilinda nchi wanachama wa NATO ambazo hazitengi bajeti ya kutosha kwa ajili ya ulinzi,” rais wa Marekani amewaambia waandishi wa habari kutoka Ikulu ya White House. Nchi wanachama wa Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini “zinapaswa kulipa zaidi,” amesisitiza.
“Tatizo langu kubwa na NATO […] ni kwamba iwapo Marekani ilikuwa na tatizo tukaita Ufaransa au nchi nyingine ambazo sitazitaja na kusema ‘tuna tatizo’, unadhani wangekuja kutusaidia, kama wanavyotakiwa kufanya? “Sina uhakika na hilo…” Rais wa Marekani pia amesema.
Kwa upande wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemjibu mwenzake wa Marekani. Amesema Ufaransa ni “mshirika mwaminifu na mtiifu.” “Siku zote tumekuwa pale kwa kila mmoja. “Sisi ni washirika waaminifu na watiifu,” Emmanuel Macron ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano maalumu huko Brussels. Amesisitiza kuwa Ufaransa imeonyesha “heshima na urafiki” kwa Marekani na viongozi wake na “inayo haki ya kudai vivyo hivyo.”
Kwa miongo kadhaa, nchi za Ulaya kwa kiasi kikubwa zimekabidhi gharama ya usalama wao, iliyotolewa na Washington ndani ya mfumo wa NATO, kwa Marekani na kupunguza matumizi yao ya kijeshi.
Marekani, ambayo ilitumia karibu 3.3% ya Pato la Taifa katika ulinzi mwaka 2024, imekuwa ikikosoa udhaifu wa matumizi ya kijeshi ya Ulaya kwa miaka kadhaa. Donald Trump alisema mwezi Januari kwamba anaamini nchi wanachama wa NATO zinapaswa kutumia 5% ya Pato lao la Taifa kwa ulinzi.