Naibu Kamanda wa IRGC: Jibu la Iran kwa mauaji ya Haniyeh litakuwa ‘tofauti, la kushangaza’ na la wakati muafaka’

Naibu Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) ameonya kuwa jibu la Tehran kwa mauaji ya Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas aliyeuawa kigaidi mjini Tehran, litakuwa tofauti na la kushangaza.