
Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, Aprili 17, mshauri mkuu wa Donald Trump kwa Afrika ametoa taarifa kuhusu ziara yake ya hivi majuzi katika bara hilo, ambayo ilimpeleka hadi DRC, Rwanda, Uganda na Kenya.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Akiwa na Corina Sanders, Naibu Katibu Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika, Massad Boulos amechukua fursa hiyo kutoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda katika eneo la Kongo, kukemea uungaji mkono wa kijeshi wa Kigali kwa M23, na kuthibitisha kuwepo kwa majadiliano kuhusu makubaliano ya uchimbaji madini kati ya Kinshasa na Washington.
Kufuatia ziara ya Massad Boulos katika eneo la Maziwa Makuu, iliyompeleka DRC, Rwanda, Uganda, na Kenya kati ya Aprili 2 na 9, msimamo wa Marekani kuhusu mzozo unaowatenganisha Wakongo wa Mashariki bado haujabadilika. “M23 lazima waweke silaha chini na majeshi ya Rwanda lazima yaondoke katitka ardhi ya Kongo. Huu ni msimamo wetu, ni wazi kabisa. “Tumeeleza wazi na tutaendelea katika mwelekeo huu,” almesema mjumbe wa Marekani kwa Afrika wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo hakumung’unya maneno yake siku ya Alhamisi, Aprili 17.
Akitoa wito kwa Kigali “kusitisha uungwaji mkono wote wa kijeshi kwa M23,” pia amesema anaamini katika suluhu la mgogoro hivi karibuni: “Nina hakika kwamba pande zinazohusika zitatafuta njia za kufikia suluhu haraka.”
Wakati msimamo huu wa utawala wa Trump si wa kimapinduzi hadi sasa, kama unavyoendana na ule wa utawala wa Biden, Massad Boulos, kwa upande mwingine, amedhihirisha jambo jipya kwa kufichua nia ya Washington ya kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na Kinshasa, haswa kupitia kusainiwa kwa makubaliano ya madini ambayo yanajadiliwa hivi sasa. Lengo: kupanua uwepo wa sekta binafsi ya Marekani katika Afrika kwa upande mmoja; na kuvutia kampuni zinazofafanuliwa kama za “kiraia”, zinazoheshimu sheria za kijamii, mazingira na kifedha za kampuni zingine.
“Makubaliano yenye faida kwa pande husika”
“Lengo ni kuwezesha uwekezaji wa kibinafsi huku ikitoa msaada wa kina: Marekani ina majukwaa kadhaa kama vile DFC, Benki ya Exim na taasisi zingine tayari kusaidia sekta ya kibinafsi” barani, ameelezea mjumbe wa Donald Trump, ambaye pia amebainisha kuwa makubaliano mengine ya aina hiyo yanatarajiwa katika kanda hiyo.
“Haya ni makubaliano yenye kubwa kwa pande mbili: : inahusu kuleta, kwa kufuata viwango, thamani iliyoongezwa kwa DRC,” ameongeza Massad Boulos ambapo Marekani pia inataka kusaidia maendeleo ya miundombinu nchini: mitambo ya kuzalisha umeme na njia za reli miongoni mwa mengine, ukanda wa Lobito ukibaki kuwa kipaumbele.
Katika mkakati huu ambapo shinikizo la kidiplomasia na matoleo ya kiuchumi yanaingiliana, Washington hata hivyo haiachi siasa. “Tuko kwenye mazungumzo na pande [zote]. “Tumefurahia pia mazungumzo kati ya utawala wa Rais Tshisekedi na M23: ni jambo la manufaa sana,” hatimaye ametangaza Massad Boulos, ambaye amekaribisha kuondoka kwa M23 kutoka Walikale-Center kama ishara ya kwanza ya kujiridhisha katika mzozo huo.