Mzozo Mashariki mwa DRC: Je, mazungumzo kati ya Kinshasa na M23 yatazaa matunda ?

Hili ni moja ya masuali mengi wengi wanajiuliza kuhusu mazungumzo kati ya DRC na waasi wa M23. Haya ni baada ya ofisi ya rais wa Angola kutangaza kwamba mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi la M23 yatafanyika Luanda hivi karibuni.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi

Mkutano kati Rais wa Kongo Félix Tshisekedi na mwenzake wa Angola, João Lourenço, mpatanishi wa mgogoro mashariki mwa DRC siku ya Jumanne, Machi 11, mjini Luanda ulilenga kutafutia suluhu mgogoro katika eneo la DRC. Mwishoni mwa mkutano huo, Angola ilitangaza kuwa majadiliano yanaweza kuanza kati ya Kinshasa na kundi la waasi la M23.

Ofisi ya rais wa Angola ilieleza kwenye mitandao ya kijamii kwamba “itaanzisha mawasiliano na M23 na ili ujumbe wa DRC na M3 waanze mazungumzo ya moja kwa moja katika siku zijazo mjini Luanda, nchini Angola” ​​, kwa nia ya kujadili amani ya uhakika katika nchi hii ndugu.”

Kinshasa “inazingatia” “mbinu ya Angola”

Kwa upande wa Kinshasa, ambapo tangu kuanza kwa mzozo huo, majadiliano haya ya moja kwa moja na kundi la waasi yamekuwa mstari mwekundu, wanahakikisha kwamba “wanazingatia” na kusubiri kuona “utekelezaji wa mbinu hii ya Angola”, amebainisha Tina Salama, msemaji wa ofisi ya rais wa Kongo, ambaye anasema kuwa tayari kuna mfumo wa mazungumzo katika mchakato unaoitwa Nairobi. Hadi sasa – Rais Tshisekedi tayari amerudia hili mara kadhaa – DRC daima imekuwa ikizingatia kwamba mazungumzo yoyote ya aina hii yanapaswa kufanyika na Rwanda, ambayo rais wa Kongo aliishtumu M23 kama kibaraka wa Rwanda mwishoni mwa mwezi wa Februari.

Tangazo hili la Angola linakuja katika mkesha wa matukio mawili muhimu: mkutano wa kilele wa kanda ya Kusini mwa Afrika kuhusu DRC leo Jumatano, Machi 12, na mkutano mpya wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo mashariki mwa DRC, Aprili 4.