Mzozo Mashariki mwa DRC: Canada yachukua hatua za kiuchumi dhidi ya Rwanda

Canada imetangaza mapema wiki hii, siku ya Jumatatu, Machi 3, 2025, hatua za kiuchumi zinazohusiana na “ushiriki wa Rwanda katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.” Rwanda imejibu vikali kuhusu hatua ya Canada ya kusitisha biashara zake.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Canada haitatoa tena leseni za usafirishaji wa bidhaa na teknolojia zinazojulikana kama zinadhibitiwa kwenda Rwanda. Pia inasitisha shughuli zingine za kibiashara za serikali kwa serikali. Ottawa pia haitaunga mkono tena shughuli za maendeleo ya biashara ya sekta ya kibinafsi au misheni rasmi ya biashara. Ushiriki wa Rwanda katika matukio yajayo yanayoandaliwa nchi Rwanda au na Rwanda pia utapitiwa upya.

Vikwazo ambavyo vinapaswa kuwa na athari ndogo, kwa sababu mahusiano ya kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili ni ya kawaida. Mnamo mwaka 2023, biashara ya kiuchumi ya nchi mbili katika bidhaa ilifikia zaidi ya dola bilioni 13.4. Ottawa inaagiza kahawa, vikolezo na viungo. Canada husafirisha ngano, magari na sehemu za spea na vipuli vya ndege kwenda Rwanda. Shirika lake la ndege la taifa la RwandAir linatumia ndege nne za Bombardier. Makampuni ya Canada yanafanya kazi nchini Rwanda hasa katika miundombinu, huduma za uhandisi, madini na sekta za nishati.

Canada inaungana na kundi dogo la matiafa kuchukua hatua dhidi ya Kigali. Katika taarifa ya pamoja, wizara tatu – Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa, na Waziri wa Ukuzaji wa Mauzo ya Nje, Biashara ya Kimataifa na Maendeleo ya Kiuchumi ya Canada, zinaonyesha “ukiukwaji wa wazi wa Rwanda wa uhuru na uadilifu wa eneo la DRC.” Canada pia inatangaza dola milioni 15 kushughulikia mahitaji ya kibinadamu Mashariki mwa DRC.

Siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imejibu uamuzi huo wa Canada katika taarifa, ikisema kwamba “hatua dhidi ya Rwanda iliyotangazwa na Canada haitatatua mzozo huo. […] Canada haiwezi kukaribisha juhudi za wahusika wa kikanda katika mchakato wa amani wakati inalaumu kila aina ya ukiukaji unaodaiwa kufanywa na Rwanda,” taarifa hiyo inasema.