Myanmar: Zaidi ya watu 1, 600 wamefariki katika tetemeko la ardhi

Watu zaidi ya 1,600 wamepoteza maisha, kufikia siku ya Jumamosi nchini Myanmar kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lilitokea katika maeneo mengi ya nchi na hata kuathiri mataifa jirani ambapo watu tisa wameuawa nchini Thailand na wajenzi karibu 100 hawajapatikana.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu wengine wamejeruhiwa nchini Mynmar kufuatia tetemeko hilo la ardhi, huku mamia wakiwa bado wamekwama kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Barabara pia zimeharibiwa kwenye tetemeko hilo la ardhi
Barabara pia zimeharibiwa kwenye tetemeko hilo la ardhi AP

Inahofiwa kuwa idadi ya maafa itaongezeka wakati huu, maafisa wa uokoaji wanapoendelea na jitihada za uokozi, kuwatafuta mamia ya watu ambao hawajapatikana.

Tetemeko hilo la ardhi liliharibu majengo, na barabara katika majimbo mbalimbali huku uogozi wa kijeshi akiomba msaada wa nchi mbalimbali kuwasaidia watu wake.

Inahofiwa kwamba huenda watu wengine wangali wamekwama kwenye vifusi vya majengo yalioporomoka
Inahofiwa kwamba huenda watu wengine wangali wamekwama kwenye vifusi vya majengo yalioporomoka REUTERS – Athit Perawongmetha

China, Marekani, India na Korea Kusini ni miongoni mwa nchi ambazo zimeanza kutuma misaada kama vyakula, dawa na hata fedha kuisadia Mynmar kipindi hiki kigumu.

Nchini Thailand, watalaam wa uokoaji wamesema wanawatafuta  watu waliokwamama kwenye jengo la ghorofa lililiporomoka jijini Bangkok, baada ya kubainika kuwa bado wako hai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *