Myanmar na Thailand zatangaza hali ya dharura kutokana na tetemeko la ardhi

Mamia ya watu wamehofiwa kupoteza maisha nchini Myanmar na Thailand, huku wengine wakikwama kwenye vifusi baada ya jengo la orofa kuporomoka jijini Bangkok.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Watalaam wa jiolojia wameripoti kuwa, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa ritcha 7.7 limetokea katika maeneo ya katikati ya nchi ya Mynmar na kusikika hadi mataifa jirani, ikiwemo Thaland.

Janga hili limesababisha serikali ya kijeshi nchini Myanmar kutangaza hali ya hatari katika majimbo sita, huku idadi ya watu waliopoteza maisha, ikiwa haijafahamika, lakini maafisa wanasema wanahofia mamia wameuawa.

Katika maeneo mbali ya nchi ya Mynmar, likiwemo jiji kuu Yangon,  majengo, barabara zimeporomoka baada ya janga hilo.

Nchini Thailand, jengo lililokuwa linajengwa limeporomoka jijini Bangkok, na wafanyakazi 81 hawajapatikana kwa mujibu wa maafisa wa serikali.

Bangkok ni jiji lenye wakaazi Milioni 17 na wengi wao wanaishi kwenye majengo marefu, ambayp yameathiriwa na tetemeko hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *