Mwili wa Shiri Bibas wakabidhiwa Israeli kabla ya mateka wengine kuachiliwa

Kipindi kipya cha mvutano ndani ya mfumo wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israeli na Hamas. Baada ya kukabidhiwa kwa mamlaka ya Israel mwili ambao haukuwa wa mateka Shiri Bibas siku ya Alhamisi, hatimaye Hamas, imekabidhi usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi Februari 22, mwili ambao umetambuliwa kuwa wa Shiri Bibas. Aliuawa akiwa uhamishoni pamoja na wanawe wawili wa kiume Ariel na Kfir, wenye umri wa miaka 4 na miezi minane mtawaliwa, wakati baada ya kutekwa Oktoba 7, 2023.

Imechapishwa:

Dakika 2

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

“Jana usiku mwili wa Shir, mpendwa wetu ulirejeshwa nyumbani,” familia ya Bibas imeandika katika taarifa siku ya Jumamosi. “Kufuatia mchakato wa utambulisho […], tulipokea asubuhi ya leo habari iliyotutia fofu sana: Mpendwa wetu, Shiri, aliuawa akiwa kizuizini,” taarifa hiyo inaongeza. “Kwa muda wa miezi 16 tumekuwa tukitafuta uhakika, na kwa kuwa sasa tunazo habari mbaya, hii haileti faraja.”

Siku ya Ijumaa mamlaka ya Israeli ilishutumu vikali kurejeshwa kwa mwili ambao haukuwa wa Shiri Bibas pamoja na watoto wake wawili, na kusababisha mshtuko na wakati mwingine hasira katika nchi ambayo hatima ya familia hii imekuwa ishara. Mwili huo ulionekana kuwa “wa mwanamke wa Kipalestina,” Gazeti la Times of Israel liliripoti.

Makabidhiano mengine leo Jumamosi

Akikemea “ubeberu usiofikirika”, Benjamin Netanyahu ameahidi kuchukua hatua “kwa dhamira ya kuwarudisha Shiri nyumbani pamoja na mateka wetu wote, walio hai na waliofariki” na kwa Hamas “kulipa bei ya ukiukaji huu wa kikatili na potovu wa makubaliano” ya usitishaji vita unaotekelezwa huko Gaza.

Hamas, ambayo ilidai mama huyo na watoto wake wawili waliuawa katika shambulio la bomu la Israeli mnamo Novemba 2023, ilikiri “kosa linalowezekana” kabla ya kukabidhi mwili mwingine kwa shirika la Msalaba Mwekundu jana usiku.

Ni wakati muafaka kuruhusu kuachiliwa tena kwa mateka wa Kipalestina na wafungwa wa Kipalestina. Hamas na Israeli watafanya mabadilishano ya saba leo Jumamosi.Hamas ilmebainisha kwamba itawaachilia mateka sita wa Israel kama ilivyopangwa Jumamosi, mateka wa mwisho walio hai ambao wanatakiwa kuwa wamerejea nchini Israel ifikapo Machi 1, wakati awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza itakapomalizika.

Kwa mujibu wa Jukwaa la Familia za Mateka, mateka ambao Hamas na makundi washirika yenye silaha watawakabidhi shirika la Msalaba Mwekundu huko Gaza, kabla ya uhamisho wao kwenda Israeli, ni Eliya Cohen, Tal Shoham, Omer Shem Tov, Omer Wenkert, waliotekwa nyara mnamo Oktoba 7, pamoja na Hisham al-Sayed na Avera Mengistu, wote wawili mateka kwa takriban miaka kumi.

Tangu kuanza kwa usitishwaji mapigano hayo, mateka 22 wa Israeli – wakiwemo watatu waliofariki – wamekabidhiwa kwa Israeli hadi sasa, ili kubadilishana na kuachiliwa kwa zaidi ya wafungwa 1,100 wa Kipalestina. Jumla ya mateka 33, wakiwemo wanane waliofariki, watabadilishwa na Wapalestina 1,900 wanaoshikiliwa na Israeli ifikapo Machi 1.

Klabu ya Wafungwa wa Palestina, shirika linalohusika na kesi hiyo, limetangaza kuwa wafungwa 602 wa Kipalestina wanatarajiwa Jumamosi, wakiwemo 50 waliohukumiwa kifungo cha maisha. Wafungwa mia moja na wanane watafukuzwa katika maeneo ya Palestina, imesema.