Mwigizaji Fredy afariki dunia akipatiwa matibabu Mloganzila

Mwigizaji wa Bongo Movie Fredy Kiluswa amefariki dunia leo Novemba 16, 2024 akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mloganzila.

Taarifa hiyo  imethibitishwa na mwigizaji mwenzie Blandina Changula ‘Johari’ wakati akizungumza na Mwananchi.

“Siwezi hata kuongea chochote, lakini taarifa za kifo ni kweli amefariki leo akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali Mloganzila, 
“amesema Johari ambaye alikuwa mzalishaji wa tamthilia ya ‘Lawama’ ambayo Fredy amewahi kucheza.

Kufuatia taarifa ya kifo cha mwigizaji huyu wasanii mbalimbali wametoa pole kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii

“Eheeeee jamaniiii mdogo wangu wewe jamanii umeondoka kweli umeondoka jamaniii Mungu wewe jamaniii ohoo Fred pumzika kwa amani wewe,”ameandika Rose Ndauka kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Lala salama kaka tutaonana baadaye kaka Uwezo wako kwenye tasnia umeonekana, unalala kwa heshima namaliza kwa kusema tasnia Filamu Tanzania na hili letu,” ameandika Steve Nyerere

“Daaah mwaka mzito huu pumzika kwa amani mdogo wangu,” ameandika JB kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Enzi za uhai wake Fredy alicheza tamthilia mbalimbali ikiwemo ya Lawama, Mizani ya Mapenzi na nyingine nyingi.