Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Severini Mushi amepongeza pendekezo la Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba la kufuta kifungu cha 3(4) cha Sheria ya Utoaji Leseni za Biashara kilichozipa mamlaka za utoaji wa leseni uwezo wa kufunga biashara iwapo mfanyabiashara atakiuka masharti ya sheria, ni zuri na litawafanya wafanyabiashara kufanya kazi kwa utulivu na amani.
✍Juliana James
Mhariri | @moseskwindi
#AzamTVUpdates