Mwenyekiti CCM asema wanafunzi wafundishwe kilimo kukabili ukosefu wa ajira

Mbeya. Ili kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana nchini, walimu wametakiwa kuweka nguvu katika somo la kilimo kuwasaidia wanafunzi wanaohitimu elimu ya sekondari na kuendelea.

Hayo yamesemwa Februari 14 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge, wakati wa kuweka jiwe la msingi katika maabara tatu za kisasa katika Shule ya Sekondari Ivumwe inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi (CCM).

Mwalunenge amesema kwa sasa ipo changamoto kubwa ya ajira kwa vijana nchini, ambapo Serikali imeweka nguvu kubwa katika kilimo, hivyo iwapo wanafunzi wataandaliwa vyema wanaweza kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Pia amewahakikishia walimu wanaofundisha shule za jumuiya hiyo kutoingiliwa majukumu yao ya kitaaluma, akiwaomba kuendelea kutekeleza wajibu wao, akisema kuwa CCM inaamini shule hizo zinaweza kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu.

“Niwapongeze uongozi wa shule hii kuanzia matokeo hadi kwenye miundombinu, niwahakikishie kwamba hakuna usumbufu mtakaopata na nielekeze viongozi wa siasa maeneo yote ya mkoa kutoingiza siasa kwenye shule hizi.”

“Kuhusu gharama za umaliziaji wa maabara hizi tatu Sh50 milioni, andaeni haraka harambee tutafute hicho kiasi na cha ziada kwa ajili ya maboresho ya madarasa na ofisi nyingine,” amesema Mwalunenge.

Amefafanua kuwa mpango wa chama hicho taifa ni kuona shule hizo zinaendelea kufanya vizuri na kipo tayari kusapoti kuhakikisha malengo yanafikiwa.

Diwani wa Kata ya Mwakibete, Lucas Mwampiki, ameahidi barabara yenye urefu wa kilomita 1.7 inayoenda shuleni hapo kujengwa kwa kiwango cha lami na kufungwa taa, akieleza kuwa tayari halmashauri imekubali kutenga bajeti.

“Tumekuwa katika ushirikiano mzuri na shule hii katika kuboresha miundombinu, lakini habari njema ni kwamba barabara yetu inayokuja hapa shuleni itajengwa kwa lami na kufungwa taa,” amesema diwani huyo.

Mkuu wa shule hiyo, Oscar Mwaihabi, amesema iwapo walimu watapewa uhuru katika majukumu yao bila kuingiliwa, shule hizo zinaweza kufanya makubwa, huku akieleza namna Ivumwe inavyobadilika kitaaluma.

Ameongeza kuwa, pamoja na changamoto zinazoikumba shule hiyo, hasa uchakavu wa madarasa na maabara, lakini uongozi umekuwa ukipambana ikiwa ni pamoja na kujenga madarasa nane ya kisasa na maabara zinazoendelea na ujenzi.

“Michango yote ya ujenzi wa miundombinu hii ni ada za wanafunzi ambapo hadi walimu wameweza kutumia sehemu ya mishahara yao kuchangia. Shule imeendelea kubadilika kitaaluma na kuwa kinara katika matokeo ya kidato cha nne na sita.”

“Kwa miaka miwili mfululizo tumefuta daraja la nne na sifuri kwa matokeo ya kidato cha nne na sita, na tunataka daraja la tatu lifutike japokuwa uchakavu wa madarasa na maabara unatupa changamoto. Kwa sasa inahitajika zaidi ya Sh50 milioni kukamilisha ujenzi huu,” amesema Mwaihabi.

Mmoja wa wazazi, Wivina Mwampashi amesema shule hiyo imekuwa kielelezo bora katika kata hiyo, akibainisha kuwa iwapo uongozi utaendelea kuaminiwa mafanikio yatakuwa makubwa, hasa kwa ufaulu wa wanafunzi.

“Mara nyingi walimu wanakatishwa tamaa ama kwa masilahi au kuhamishwa vituo. Mfano, huyu mwalimu mkuu ameonyesha mabadiliko makubwa. Aaminiwe atupeleke katika mafanikio zaidi tuone ushindani wa shule hizi na zile nyingine,” amesema Wivina.

Ili kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana nchini, walimu wametakiwa kuweka nguvu katika somo la kilimo kuwasaidia wanafunzi wanaohitimu elimu ya sekondari na kuendelea.

Hayo yamesemwa leo Februari 14 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge wakati wa kuweka jiwe la msingi katika maabara tatu za kisasa katika shule ya Sekondari Ivumwe inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi (CCM).

Mwalunenge amesema kwa sasa ipo changamoto kubwa ya ajira kwa vijana nchini, ambapo serikali imeweka nguvu kubwa katika kilimo hivyo iwapo wanafunzi wataandaliwa vyema wanaweza kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Pia amewahakikishia walimu wanaofundisha shule za Jumuiya hiyo kutoingiliwa majukumu yao ya kitaaluma akiwaomba kuendelea kutekeleza wajibu wao akisema kuwa CCM inaamini shule hizo zinaweza kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu.

“Niwapongeze uongozi wa Shule hii kuanzia matokeo hadi kwenye miundombinu, niwahakikishie kwamba hakuna usumbufu mtakaopata na nielekeze viongozi wa siasa maeneo yote ya Mkoa kutoingiza siasa kwenye shule hizi”

“Kuhusu gharama za umaliziaji wa maabara hizi tatu Sh50 milioni, andaeni haraka harambee tutafute hicho kiasi na cha ziada kwa ajili ya maboresho wa madarasa na ofisi nyingine” amesema Mwalunenge.

Amefafanua kuwa mpango wa Chama hicho Taifa ni kuona shule hizo zinaendelea kufanya vizuri na kipo tayari kusapoti kuhakikisha malengo yanafikiwa.

Diwani wa Kata ya Mwakibete, Lucas Mwampiki ameahidi barabara yenye urefu wa kilomita 1.7 inayoenda shuleni hapo kujengwa kwa kiwango cha lami na kufungwa taa akieleza kuwa tayari Halmashauri wamekubali kutenga bajeti.

“Tumekuwa katika ushirikiano mzuri na shule hii katika kuboresha miundombinu, lakini habari njema ni kwamba barabara yetu inayokuja hapa shuleni itajengwa kwa lami na kufungwa taa” amesema Diwani huyo.

Mkuu wa Shule hiyo, Oscar Mwaihabi amesema iwapo walimu watapewa uhuru katika majukumu yao bila kuingiliwa, shule hizo zinaweza kufanya makubwa huku akieleza namna Ivumwe inavyobadilika kitaaluma.

Ameongeza kuwa pamoja na changamoto zinazoikumba shule hiyo haswa uchakavu wa madarasa na maabara lakini uongozi umekuwa ukipambana ikiwa ni kujenga madarasa nane ya kisasa na maabara zinazoendelea na ujenzi.

“Michango yote ya ujenzi wa miundombinu hii ni ada za wanafunzi ambapo hadi walimu wameweza kutumia sehemu ya mishahara yao kuchangia, shule imeendelea kubadilika kitaaluma na kuwa kinara katika matokeo ya kidato cha nne na sita”

“Kwa miaka miwili mfululizo tumefuta daraja la nne na sifuri kwa matokeo ya kidato cha nne na sita na tunataka daraja la tatu lifutike japokuwa uchakavu wa madarasa na maabara unatupa changamoto, kwa sasa inahitajika zaidi ya Sh50 milioni kukamilisha ujenzi huu”  amesema Mwaihabi.

Mmoja wa Wazazi, Wivina Mwampashi amesema shule hiyo imekuwa kielelezo bora katika Kata hiyo, akibainisha kuwa iwapo uongozi utaendelea kuaminiwa mafanikio yatakuwa makubwa haswa kwa ufaulu wa wanafunzi.

“Mara nyingi walimu wanakatishwa tamaa aidha kwa maslahi na kuhamishwa vituo, mfano huyu mwalimu Mkuu ameonesha mabadiliko makubwa, aaminiwe atupeleke katika mafanikio zaidi tuone ushindani wa Shule hizi na zile nyingine” amesema Wivina.