
Rais wa DRC Fekix Thisekedi wakati akihudhuria mkutano wa usalama mjini Munich Ujerumani, alikutana na mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, Karim Khan.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wawili hao walijadiliana kuhusiana na ushuhuda ambao mahakama hiyo imepata katika uchunguzi wake wa makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu yanayotekelezwa mashariki ya DRC.
Mwendesha mashataka wa ICC anatarajiwa kuzuru DRC mwishoni mwa mwezi huu wa Februari kuendeleza uchunguzi wake dhidi ya uhalifu unaotekelezwa dhidi ya binadamu.
Khan na Thisekedi walibakuliana kwamba ni lazima haki itendeke dhidi ya wahusika wote wanaotekeleza uvamizi dhidi ya raia wa mashariki ya DRC.
Rais Thisekedi pia alizungumza na rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier kuhusu haja ya Rwanda kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kama njia moja ya kuanchana na uvamizi wake mashariki ya DRC.
Baada ya ziara yake mfupi ya kikazi nchini Ujerumani, Rais Thisekedi anatarajiwa kurejea jijini Kinshasa wakati huu waasi wa M23 wakiripotiwa kuingia katika Mji wa pili kwa ukubwa wa Bukavu, Kivu Kusini.