Mwanasiasa mwenye chuki dhidi ya Uislamu Denmark avunjia heshima Qur’ani

Mwanasiasa mwenye uraia pacha wa Sweden na Denmark na mwenye chuki dhidi ya Uislamu, Rasmus Paludan kwa mara nyingine tena ameivunjia heshima Qur’ani Tukufu kwa kuchoma moto nakala ya kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen.