
Kati ya wanaharakati 12 waliokuwa kwenye boti ya Madleen, iliyokuwa imebeba chakula na vifaa kuelekea Gaza, wanne akiwemo Thunberg walikubali kufukuzwa mara moja, huku wote wakipigwa marufuku ya kutokanyaga Israel kwa miaka 100.
Shirika la haki za binaadamu la Adalah limesema wanaharakati wanane waliosalia waliwekwa kizuizini baada ya kukataa kuondoka Israel kwa hiari, na kufikishwa mbele ya jopo la kufanya tathmini ya kukamatwa kwao. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema wanaharakati wanne kutoka Ufaransa ambao pia walikuwa kwenye boti hiyo ya Madleen wanatarajiwa kufikishwa mbele ya jaji wa Israel.
Alipoulizwa alipowasili Stockholm ikiwa alikuwa na hofu wakati vikosi vya usalama vya Israel vilipoingia kwenye boti ya, Thunberg mwenye umri wa miaka 22 alijibu kuwa anachoogopa ni kwamba watu wako kimya wakati mauaji ya kimbari yanayendelea huko Gaza.