Mwanafunzi wa Iran ashinda ‘Tuzo ya Mtafiti Kijana wa Mwaka’ ya BRICS na SCO

Hosna Salimi, mwanafunzi wa Kiirani wa Kitivo cha Taaluma za Dunia (FWS) cha Chuo Kikuu cha Tehran ameshinda Tuzo ya ‘Mtafiti Kijana Bora wa Mwaka’ katika taasisi ya BRICS na Tuzo ya Viongozi Vijana ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa mwaka 2025 kutokana na kazi bora aliyofanya katika sayansi na utafiti.