Akiwa amevutiwa na ahadi za maisha bora ya baadaye nchini Urusi, mwanafunzi kutoka Togo Dosseh badala yake alijikuta katika uwanja wa vita – akiwa amepigwa risasi, kufungwa gerezani na kusahaulika. Sasa, familia yake na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yanapigania uhuru wake.