Mwanadiplomasia wa zamani wa US: Jinai za Ghaza ‘zitamsakama’ Blinken hadi mwisho wa maisha yake

Mwanadiplomasia wa Marekani aliyejiuzulu mwaka jana kulalamikia vita vya Ghaza na uungaji mkono wa Washington kwa vita hivyo amesema, jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika vita hivyo ‘zitamsakama’ waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Antony Blinken kwa muda wote uliosalia wa maisha yake.