Mwanadiplomasia: Kuna mawasiliano yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na watawala wa Syria

Mjumbe maalum wa waziri wa mambo ya nje wa Iran katika masuala ya Syria amethibitisha kwamba Iran ina mawasiliano yasiyo ya moja kwa moja na kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) linalotawala Syria, zaidi ya miezi miwili baada ya kundi hilo la wanamgambo kuchukua mamlaka katika nchi hiyo ya Kiarabu.