Mwana wa Nasrullah asema siku ya Jumapili ya mazishi ya baba yake ni “Siku ya Kutangaza Msimamo”

Sayyid Muhammad Mahdi Nasrullah, mwana wa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon aliyeuawa shahidi amesema katika hotuba ya kuwaalika watu kuhudhuria mazishi ya baba yake kwamba: “kushiriki katika mazishi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah kutakuwa ni kushiriki katika siku ya kutangaza msimamo wa mtu na kudhihirisha kivitendo mapenzi kwa Shahidi Nasrullah”.