Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi awasalia Mashahidi wa Hizbullah, bahari ya umati wa watu yaifunika Beiru

Sheikh Muhammad Yazbek, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongoza Sala ya Maiti ya kusalia miili ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyyuddin katika mazishi ya kihistoria yaliyofanyika leo katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.