Mvutano wazuka kati ya Misri na Marekani baada ya tishio la Trump; el Sisi ‘huenda akaashirisha’ ziara ya Washington

Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi huenda akaahirisha ziara yake iliyokuwa imepangwa mjini Washington, kama ishara ya mkwamo mkubwa wa kidiplomasia wakati huu kukiwa na mvutano unaoongezeka kati yake na Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mgogoro wa Gaza na vitisho vya kukata misaada ya Washington kwa serikali ya Cairo.