Muungano wa nchi za Kiarabu wapinga uwepo wa serikali mbadala Sudan

Muungano wa nchi za Kiarabu, umesema jaribio lolote la kuanzisha serikali mbadala nchini Sudan halikubaliki na kwamba njia pekee ni kwa pande zinazohusika kuzungumza ili kumaliza tofauti zao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa muungano huo, balozi Jamal Rushdi, amesema wakuu wa nchi siku ya Jumamosi kwa kauli moja walitangaza kuiunga mkono Serikali ya kijeshi na kutupilia mbali mpango wowote wa kuunda serikali mbadala.

Kwenye taarifa yao ya pamoja baada ya kutamatika kwa mkutano wao mwishoni mwa juma lililopita, wakuu hao wa nchi walisisitiza umuhimu wa kutafuta suluhu kwa njia ya amani huku wakitaka kuheshimiwa kwa mipaka na uhuru wa taifa hilo kujitawala.

Aidha kwa upande wake serikali ya Sudan iliyowakilishwa na mjumbe wa baraza la mpito, Ibrahim Jaber, alisema Khartoum inaunga mkono mpango wa amani wa umoja wa Mataifa, ambao unataka kusitishwa kwa vita, wapiganaji wa RSF kuondoka katika maeneo inayoyakalia pamoja na kurejea kwa wakimbizi.

Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, amesema nchi ya Sudan iko katika hali mbaya na kwamba kunahitajika juhudi za haraka kukomesha vita na kurejesha utulivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *