Katika msimu wa joto wa 2013, mmiliki wa mgahawa wa Moscow alipigwa risasi katika mji mkuu wa Urusi. Mwanamume aliyevalia kofia aliruka kutoka kwenye baiskeli na kumpiga risasi mara mbili kabla ya kukimbia
Miaka sita baadaye, kamanda wa Chechnya aliyekimbilia uhamishoni Zelimkhan Khangoshvili, aliuawa katika bustani ya Berlin yenye shughuli nyingi katika hali kama hiyo ya kutisha, akipigwa risasi na mtu aliyekuwa kwenye baiskeli kutumia bastola ya Glock 26 mchana peupe.
Mshambulizi huyo alikamatwa baada ya kutupa bastola na wigi kwenye mto Spree karibu na Reichstag, jengo la bunge la Ujerumani.
Pasipoti iliyo na jina “Vadim Sokolov” ilipatikana kwa muuaji wa Berlin, lakini viongozi waligundua haraka kuwa hilo halikuwa jina lake.
Mwanamume mwenye kipara, waliyemkamata alikuwa ni Vadim Krasikov, raia wa Urusi ambaye ana uhusiano na FSB, idara ya usalama ya Urusi – na mshukiwa mkuu wa mauaji ya 2013 huko Moscow.
Baada ya kumnyemelea na kumpiga risasi Khangoshvili katika Hifadhi ya Kleiner Tiergarten, Krasikov alitupa baiskeli yake, bastola, na begi lililokuwa na sura yake ndani ya Mto Spree. Mashahidi waliwaita polisi, ambao walimzuilia. Kisha wachunguzi walipata alama za vidole vyake kwenye baadhi ya vitu vilivyochukuliwa na wapiga mbizi wa polisi. Krasikov alikanusha mauaji hayo, akisema kwamba alikuwa mtalii anayeitwa Vadim A. Sokolov, jina lililo kwenye pasipoti yake ya Urusi. Utambulisho wake halisi hatimaye ulianzishwa kwa kutumia picha zilizoonyesha tatoo zake za kipekee. Waendesha mashtaka wa Ujerumani walionyesha kwamba Krasikov alifanya kazi katika Huduma ya Usalama ya Shirikisho la Urusi, ambayo ilimpa utambulisho wa uwongo, pasipoti, na rasilimali za mauaji.
Wachunguzi walimtambua Krasikov kwa usaidizi wa idara za usalama za Ukraine, ambaye aliona picha za mwanamume mwenye tattoo zinazofanana – akionekana kuwa pepo aliyevaa taji na nyoka – katika ndoa yake ya pili, na mwanamke kutoka mji wa Kharkiv wa Ukraine mwaka 2010.
Mauaji yaliyoidhinishwa na serikali
Vidokezo vya kwanza vya uwezekano wa mkono wa Kremlin katika mauaji ya Berlin vinatoka kwa historia ya Krasikov – au tuseme, ukosefu wa moja.
Hati zilizopatikana na tovuti ya uchunguzi ya Bellingcat zinaonyesha alikuwa akitafutwa kwa mauaji ya 2013 ya Moscow. Walakini, miaka miwili baadaye, hati ya kukamatwa iliondolewa na kitambulisho cha “Vadim Krasikov” kilionekana kutoweka.
Vadim Krasikov alikuwa wa kitengo cha siri cha ‘Vympel’ cha huduma ya siri ya Urusi, FSB, kulingana na waendesha mashtaka katika kesi yake.
“Majukumu yake rasmi ni operesheni za kukabiliana na ugaidi nyumbani, lakini kwa njia nyingi imerejea kwenye mizizi yake ya awali, kama kitengo kilichopewa jukumu la “kazi-nyevu” – hujuma na mauaji – nje ya nchi,” anasema mwanahistoria wa Putin na mtaalamu wa usalama wa Urusi Mark Galeotti .
Krasikov binafsi alikutana na Putin kwenye safu ya kulenga shabaha alipokuwa akihudumu na Vympel, akimiliki BMW na Porsche, na alisafiri kwenda kazini mara kwa mara, kulingana na mahojiano ambayo shemeji yake alitoa The Insider
Wakati huo “Vadim Sokolov”, mwenye umri wa miaka 45, alionekana. Mnamo 2015 alipata pasipoti, na, mnamo 2019, nambari ya kitambulisho cha ushuru.
Mahakama ya Ujerumani ilihitimisha kwamba hati hii inaweza tu kuidhinishwa na Kremlin, na kwa hiyo kwamba Vadim Krasikov alikuwa na msaada wa serikali kwa mauaji ya Berlin.
“Mamlaka ya serikali ya Urusi iliamuru mshtakiwa kumuua mwathiriwa,” hakimu kiongozi wa Ujerumani alisema baada ya kumhukumu Krasikov kifungo cha maisha gerezani
Mwathiriwa wake, Zelimkhan Khangoshvili, alikuwa kamanda wa waasi wa Chechnya kati ya 2000 na 2004, wakati Chechnya ilikuwa inapigana vita vya uhuru dhidi ya Urusi.
Kwa waangalizi wa Magharibi, Bw Khangoshvili alionekana kuwa sehemu ya msururu wa mauaji yaliyoamriwa na Moscow ya watu waliotoroka Chechen kwenda huko Ulaya na Mashariki ya Kati.
Kremlin ilikanusha kupanga mauaji ya Berlin, na kutupilia mbali hukumu dhidi ya Krasikov kama “iliyochochewa kisiasa”