Msumbiji: Wadau wasaini makubaliano ya kisiasa Maputo

Nchini Msumbiji, Rais Daniel Chapo na wawakilishi kadhaa wa mashirika ya kiraia, makundi ya kidini na upinzani wametia saini “mkataba wa mapatano ya kisiasa” kwa ajili ya “mazungumzo jumuishi ya kitaifa” siku ya Jumatano, Machi 5, wakati wa sherehe iliyofanyika katika mji mkuu Maputo. 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Mpango huo, ambao unalenga “kurudisha utulivu wa kisiasa na kijamii” nchini Msumbiji, unafuatia miezi kadhaa ya maandamano ya baada ya uchaguzi katika mitaa ya nchi hiyo. Hata hivyo, mpinzani Venancio Mondlane, ambaye anadai ushindi katika uchaguzi wa Oktoba, si miongoni mwa waliotia saini na kutawanywa kwa kikatili kwa maandamano siku ya hii mjini Maputo kumeibua tena mvutano.

Watia saini tisa walimzunguka Rais wa Msumbiji Daniel Chapo kwa ajili ya kupitishwa kwa “mkataba wa kisiasa” uliokuwa na upinzani mkubwa. Miongoni mwa waliotia saini mkataba huu ni Albino Forquilha, kiongozi wa chama cha Podemos, ambaye alikuwa ameunda muungano na Venancio Mondlane wakati wa uchaguzi uliopita. Lakini uamuzi wa chama hicho kuketi katika Bunge la taifa la Msumbiji ulishutumiwa kama usaliti na Venancio Mondlane, ambaye bila shaka ameachana na Podemos.

Katika hotuba yake kwenye jukwaa, Albino Forquilha alizungumza na kuunga mkono “Msumbiji iliyostawi na iliyopatanishwa”. Kiongozi wa Podemos amewataka wakazi wa Msumbiji kuonyesha “nia njema” kukomesha “migogoro” nchini humo. “Maslahi ya nchi ya Msumbiji lazima yawekwe juu ya vyama vya siasa,” Albino Forquilha amesema. Ni lazima tuchore njia kuelekea Msumbiji iliyoungana, yenye ustawi na maendeleo […]. Migogoro ya mara kwa mara katika nchi inapaswa kukomeshwa mara moja na kwa wote. Hatuwezi kuhalalisha usumbufu wa utaratibu wa umma, ambao unazuia harakati huru za watu. “

Mara tu baada yake, Rais Daniel Chapo – kutoka Frelimo – alitoa wito wa “mapatanisho” ya Wasumbiji na kulaani “maandamano ya vurugu, haramu, hata ya uhalifu” katika miezi ya hivi karibuni: “Mazungumzo haya ya kitaifa yaliyojumuisha ni nafasi ambayo raia wote wa Msumbuji wana nafasi yao, ikiwa ni pamoja na wale wanaojiita waandamanaji, iwe ni washirika wa chama au la […]. Tunatoa wito wa kuundwa na kuunganishwa kwa mfumo wa kisiasa wa vyama vingi na wa kidemokrasia katika nchi yetu.”

Maandamano ya mpinzani Mondlane yatawanywa kwa risasi za moto

Wakati huo huo, msafara wa mamia ya watu wakiongozana na Venancio Mondlane waliandamana katika mitaa ya Maputo, kabla ya maandamano hayo kukatizwa na risasi za moto na mabomu ya machozi. Wafuasi wa Venancio Mondlane walishutumu “mashambulizi ya kuvizia” dhidi ya kiongozi huyo wa upinzani. Takriban watu 16 walijeruhiwa, shirika lisilo la kiserikali la Plataforma Decide limesema.