Msumbiji: Rais Chapo akutana na kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane

Rais wa Msumbiji Daniel Chapo amekutana na kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane kwa mazungumzo ya kujaribu kutuliza wasiwasi kwenye taifa hilo kutokana na maandanao ya kupinga matokeo ya uchaguzi Mkuu wa urais.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo lenye utajiri wa mafuta la kusini mwa Afrika limeshuhudia vurugu za baada ya uchaguzi tangu mwezi Oktoba mwaka jana baada ya upinzani kukataa matokeo ya urais.

Uchaguzi huo ambao waangalizi kadhaa wa kimataifa walisema ulikumbwa na dosri, ulifuatiwa na miezi kadhaa ya maandamano ya upinzani ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 360 kwa mujibu wa mashirika ya kiraia.

Maandamano ya kupinga ushindi wa Daniel Chapo katika uchaguzi Mkuu yalifanyika jijini Maputo, Msumbiji, Tarehe 24 Oktoba 2024.
Maandamano ya kupinga ushindi wa Daniel Chapo katika uchaguzi Mkuu yalifanyika jijini Maputo, Msumbiji, Tarehe 24 Oktoba 2024. REUTERS – Siphiwe Sibeko

Chapo na Mondlane walikutana siku ya Jumapili ya wiki iliopita katika Mji mkuu wa Maputo kujadili changamoto zinazolikabili taifa hilo kulingana na taarifa kutoka ofisi ya rais.

Kulingana na taarifa hiyo, mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uthabiti wa taifa hilo pamoja na kuwaleta watu pamoja.Hadi tukichapisha ripoti hii haikuwa imeekwa wazi iwapo kutakuwa na makubaliano ya kisiasa kati ya Mondlane na rais Chapo.

Rais wa Msumbiji Daniel Chapo
Rais wa Msumbiji Daniel Chapo AFP – AMANUEL SILESHI

Rais Chapo aliingia madarakani mwezi Januari na mapema mwezi huu alitia saini makubaliano ya baada ya uchaguzi na vyama vingine tisa kikiwemo kile cha Podemos ambacho Modlane alitumia kuwania urais.

Makubaliano haya bado yanasubiri kuidhinishwa na bunge ambapo pia yanatarajiwa kupelekea kufanyika kwa mageuzi ya katiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *