
Kimbunga cha Jude kilipiga ufuo wa kaskazini mwa nchi mnamo siku ya Jumatatu, Machi 10, 2025, kikiwa na dhoruba za upepo zinazozidi kilomita 195 kwa saa. Ripoti ya hivi punde, iliyochapishwa siku ya Alhamisi na Taasisi ya Kudhibiti Maafa, inaonyesha watu 9 walifariki na 20 kujeruhiwa. Uharibifu wa nyenzo ni mkubwa. Na idadi ya vifo inaendelea kuongezeka huku mvua zikiendelea kunyesha.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kanda, Gaëlle Laleix
Kulikuwa na zaidi ya raia 200,000 wa Msumbiji walioingia gizani jana. Kulingana na Electricidad de Mozambique, mitambo katika majimbo ya Zambezi na Nampula, katikati na kaskazini mwa nchi, bado haifikiki. Shirika la kitaifa la Umeme linasikitishwa na uharibifu wa kilomita 74 za nyaya za umeme na kuanguka kwa transfoma sita.
Miundombinu mingine iliyoathirika vibaya ni pamoja na barabara na madaraja. Barabara ya taifa namba 1 katika Mkoa wa Zambezi ilikatwa vipande viwili Barabara nyingine tano ziliharibiwa katika Mkoa wa Nampula, pamoja na njia kadhaa za kupita. “Hali tunayopitia ni ya mbaya sana,” Eduardo Abdula, gavana wa jimbo la Nampula, ameambia vyombo vya habari. Wilaya zetu nyingi hazina tena mawasiliano ya simu za mezani. “
Kulingana na mamlaka, kimbunga Jude pia kiliharibu karibu shule 60, na kusababisha takriban watoto 17,500 kushindwa kuendelea na masomo. Guy Taylor, msemaji wa UNICEF nchini Msumbiji, pia anahofia magonjwa ya kipindupindu na malaria.
Hiki ni kimbunga cha tatu kukumba Msumbiji tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu, matukio haya ya Tabianchi yaliathiri takriban raia milioni 5 wa Msumbiji kati ya mwaka 2019 na 2023.