Nchini Msumbiji, kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane, amemfungulia mashtaka rais Daniel Chapo kwa kuchochea machafuko nchini humo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii ya Mondlane, imekuja huku akifika mbele ya mwanasheria mkuu wa serikali siku ya Jumanne, kujieleza kutokana na kuwa na watu wanane mashuhuri wanaoida kuchochea machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita.
Kiongozi huyo wa upinzani anadai kuwa kauli ya rais Chapo, Februari tarehe 24 akiwa katika mkoa wa Cabo Delgado kuwa atakuwa tayari kumwaga damu kulinda amani ya nchi hiyo, ni uchochezi mkubwa wa kutaka machafuko nchini humo.

Aidha, amesema matamshi ya kiongozi huyo, ni kama tangazo la vita, na yanalenga kuzuia uwezekano wowote wa kufanyika kwa mazungumzo, ili kutatua changamoto ya kisiasa katika taifa hilo.
Mondlane, ameeendelea kusisitiza kuwa maisha yake yapo hatarini, kufuatia shmbulizi la tarehe 5 mwezi huu wakati yeye na wafuasi wake walishambuliwa na maafisa wa usalama.