
Imesisitizwa katika kikao cha balozi wa Sudan nchini Iran na Mkuu wa kitengo cha matangazo ya nje cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) nia ya dhati ya nchi hizo mbili ya kuendeleza ushirikiano wa vyombo vya habari.
Abdelaziz Hassan Saleh Taha, balozi wa Sudan nchini Iran, na ujumbe huo alioandamana nao amekutana na Ahmad Noroozi, Mkuu wa kitengo cha matangazo ya nje cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na kujadili masuala mbalimbali yakiwemo kupanuliwa ushirikiano wa vyombo vya habari baina ya pande mbili.
Noroozi amesema, Iran imeonyesha kuwa inaweza kuwa rafiki mwaminifu kwa kando ya taifa na serikali ya Sudan, na hakuna shaka kwamba kuvileta pamoja vyombo vya habari vya Iran na Sudan kunaweza kuleta mafanikio makubwa.
Kwa upande wake balozi wa Sudan nchini Iran amesema: Iran na Sudan zina mambo mengi yanayofanana na zina mitazamo ya pamoja kuhusiana na muuqawama na masuala ya kidini.
Abdul Aziz Hassan Saleh Taha sanjari na kulaani jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza na Lebanon na vilevile mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Iran amesema: “Sasa mikono hiyo hiyo inayowaua watu huko Gaza inazusha machafuko na migogoro nchini Sudan.