Mshindi wa Tuzo za SAMIA KALAMU AWARDS Ndg Mathias Canal amechangia vifaa vya michezo katika shule mbili za Msingi ambazo ni Kiomboi Bomani na Kiomboi Hospitali.
Vifaa hivyo amevikabidhi kwa Wakuu wa Shule hizo mbili ikiwemo Jezi jozi mbili za mpira wa miguu kwa kila shule, jezi jozi mbili za mpira wa pete, mipira kwa ajili ya mchezo wa Pete na mchezo wa mpira wa miguu.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo tarehe 17 Mei 2025 katika shule ya msingi Kiomboi Bomani na kuhudhuriwa na Diwani wa kata ya Kiomboi Mhe Omary Omary, Afisa Elimu kata ya Kiomboi Mwl Fabiana Mbuta, Wakuu wa shule, na walimu wakiwemo walimu wa michezo, Mathias amesema kuwa vifaa hivyo vya michezo vitakuwa chachu ya kuimarisha afya ya akili na mwili kwa wanafunzi sambamba na kuwaweka pamoja wanafunzi ili kutojiepusha na makundi ovu.
Pia, Mathias ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Iramba kuendelea kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe Mwigulu Mchemba ili aweze kutekeleza kwa ufasaha majukumu yake katika Taifa la Tanzania.
Mathias amempongeza Dkt Mwigulu kwa kushirikiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda kwa kuongeza bajeti ya wizara kutoka Trilioni 1.9 mwaka 2024/2025 hadi kufikia shilingi Trilioni 2.4 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo kuna ongezeko la zaidi ya shulingi Bilioni 500.
#StarTvUpdate