MSF yapaza sauti kuhusu kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia mashariki mwa DRC

Katika ripoti iliyochapishwa wiki hii, Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) linaonyesha wasiwasi wake kuhusu hali ambayo imezorota kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kutishwa na ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kingono lililorekodiwa, haswa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, tangu mwanzoni mwa mwaka.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetoa tahadhari tena kuhusu unyanyasaji wa kingono nchini DRC, hasa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, ambayo inakabiliwa na mzozo mkali kati ya kundi la AFC/M23 linaloungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda, na jeshi la Kongo na washirika wake. Hali hi inatia wasiwasi hasa katika mikoa hii miwili ya mashariki mwa nchi, ambapo kumekuwa na ongezeko la kutisha la ukatili wa kijinsia tangu mwanzoni mwa mwaka wa 2025, MSF inaandika katika ripoti iliyochapishwa wiki hii.

MSF pia inasema kwamba imeona hali inayozidi kuzorota katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikionyesha hasa kesi 40,000 ilizoshughulikia mwaka 2024 huko Kivu Kaskazini pekee—idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa, shirika hilo linasema. Kwa mwaka wa 2025, MSF inadai kuwa tayari imerekodi wahasiriwa 7,400 huko Goma, 2,400 huko Saké, na 700 huko Kivu Kusini. Idadi kubwa ya unyanyasaji huu wa kijinsia hufanywa na watu wenye silaha na huathiri zaidi wanawake, lakini pia kwa watoto: karibu 13% ya wahasiriwa ni watoto wadogo, shirika hilo linabainisha.

Takwimu hizi zinalingana na zile za Ofisi ya Pamoja ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, ambayo, mwezi wa Aprili, iliripoti ongezeko la zaidi ya 152% ya unyanyasaji wa kingono mashariki mwa DRC kati ya mwezi wa Januari na Februari. Wakati takwimu za mwezi Machi zinakaribia kufanana, Umoja wa Mataifa pia unaonya kuwa uwezo wake wa ufuatiliaji katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa AFC/M23 “umeathiriwa sana na ukosefu wa usalama na vikwazo vya ufikiaji.”

Wakati MSF ikibainisha hili, inasisitiza kuwa takwimu zake “hazijakadiriwa ikilinganishwa na hali halisi,” kwani upatikanaji wa huduma za afya unasalia kuwa mgumu katika eneo la mashariki mwa nchi. Shirika hilo linatoa wito kwa juhudi zaidi kusaidia waathiriwa. Sababu? Kupungua kwa ufadhili wake kufuatia serikali ya Trump kupunguza bajeti ya Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) mapema mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *