Msewa anavyoikomboa Trabzonspor

KIUNGO Mtanzania, Diana Msewa anayekipiga Trabzonspor inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini Uturuki amekuwa mkombozi kwenye kikosi hicho tangu asajiliwe msimu huu akitokea Amed SK.

Trabzonspor iko nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikishinda mechi 12 sare tatu na kupoteza sita ikikusanya pointi 39 kwenye michezo 21.

Tangu atue klabuni hapo msimu huu akitokea Amed ya nchini humo amekuwa na kiwango bora akiwa na msaada mkubwa kuanzia kuzuia na kushambulia. Katika mechi 21 alizocheza, timu hiyo imefunga mabao 39 na kuruhusu lango lake kutikiswa mara 17.

Msimu uliopita hadi raundi ya 21 chama hilo lilikuwa nafasi ya 13 kati ya 14 zinazoshiriki ligi hiyo inayoongozwa na Fenerbahce yenye pointi 55.

Hata hivyo, ilijipapatua hadi ligi inatamatika ikasogea nafasi mbili za juu na kumaliza nafasi ya 11 .

Kiungo huyo amefunga mabao matatu na asisti saba kwenye mechi 21 ilizocheza hadi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *