Mradi wa umeme wa nishati jua unaojengwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63 huku ukitarajiwa kukamilika mwis…

Mradi wa umeme wa nishati jua unaojengwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63 huku ukitarajiwa kukamilika mwis…

Mradi wa umeme wa nishati jua unaojengwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63 huku ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

Hayo yamewekwa wazi na Mkurugenzi wa Tanesco, Lazaro Twange wakati wa ziara ya kukagua mradi huo unaolenga kuchangia Megawati 50 kwenye gridi ya taifa pindi utakapokamilika.

“Awamu hii ya kwanza itaongeza nguvu ya usambazaji wa umeme kwa wananchi na tunamshukuru Rais kwakuwa tayari tumepatiwa fedha kwa ajili ya kupata mkandarasi atakayetekeleza awamu ya pili ambayo itazalisha mara mbili ya umeme utakaozalishwa na awamu hii ya kwanza” amesema Twange

Kwa upande wake meneja wa mradi huo, Emmanuel Anderson amesema mradi huo umechelewa kukamilika baada ya mkandarasi kupatwa na changamoto na serikali kupitia TANESCO kuridhia kumuongezea muda kutoka Februari hadi Oktoba, 2025.

Awamu zote mbili za mradi huo ulioanza kutekelezwa Disemba 2023 zitagharimu Shilingi Bilioni 323 na zinatarajiwa kuongeza Megawati 150 kwenye gridi ya Taifa.

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *