Mpatanishi mkuu wa Putin anaelekea Washington kwa mazungumzo na mjumbe wa Trump, vyanzo vyasema

Mpatanishi mkuu wa Kremlin anatarajiwa mjini Washington wiki hii kwa mazungumzo na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump, vyanzo viwili vinavyofahamu mpango huo vimesema. Ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Urusi kuzuru Ukraine tangu uvamizi wa Moscow mwaka 2022. 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Kirill Dmitriev, mkuu wa hazina ya fedha za kigeni ya Urusi, ambaye aliteuliwa na Rais Vladimir Putin kuwa mjumbe maalum wa uwekezaji na uchumi wa kimataifa, atakutana na mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff, chanzo kimesema kwa sharti la kutotajwa jina.

Chanzo kingine kimesema kwamba Dmitriev atakutana na Witkoff siku ya Jumatano Aprili 2.

Mkutano wao umeripotiwa mapema na CNN, ambayo imesema Dmitriev na Witkoff watafanya mazungumzo kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili wakati wanajaribu kumaliza vita nchini Ukraine.

“Labda. Upinzani dhidi ya mazungumzo ya Marekani na Urusi ni wa kweli-unaochochewa na maslahi yaliyoimarishwa na simulizi za zamani,” Dmitriev amesema  katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii X akijibu makala ya CNN.

“Lakini vipi ikiwa uhusiano ulioboreshwa ndio hasa ulimwengu unahitaji kwa usalama na amani ya kudumu ya kimataifa.”

Ikulu ya Marekani na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani hawakutoa maoni yao mara moja. Ubalozi wa Urusi huko Washington haukujibu mara moja ombi la maoni.

Safari ya Dmitriev inakuja wakati Trump anatafuta kukutana na Putin hivi karibuni ili kufanya kazi ya kurekebisha uhusiano ulioharibika na kufuatia mazungumzo ya simu ya hivi karibuni kati ya viongozi hao wawili ambao pia yalilenga kufikia makubaliano ya amani ya Ukraine.

Lakini wakati Trump akionekana kuzidi kukosa subira kwa kile alichopendekeza kuwa huenda ni kuburuza miguu kwa Moscow juu ya mapatano mapana ya amani ya Ukraine na kusema “amechukizwa” na Putin, dokezo la Dmitriev pia linaweza kupunguza baadhi ya mivutano.

Baada ya kukumbwa na vikwazo vya nchi za Magharibi kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine na kutumia vyema maoni ya Trump kuhusu kukarabati uhusiano, Urusi ina nia ya kuwarejesha wawekezaji wa kimataifa ili kuleta mseto wa uchumi wake unaoendeshwa hasa na vita katika miaka mitatu iliyopita.

Kwa vile Dmitriev bado yuko chini ya vikwazo vya Marekani, CNN imeripoti kwamba utawala wa Trump uliondoa vikwazo kwa ziara yake kwa muda.

Dmitriev, anayechukuliwa kuwa mwanachama mwenye ujuzi zaidi wa Marekani wa wasomi wa Urusi, alisema mapema wiki hii kwamba nchi hizo mbili tayari zimeanza kuzungumza mradi wa pamoja wa madini ya adimu, kati ya mikataba mingine.

Mwezi Februari Putin alipendekeza kwamba Marekani inaweza kuwa na nia ya kufanya uchunguzi wa pamoja wa amana nchini Urusi. Urusi ina akiba ya tano kwa ukubwa duniani ya metali zinazotumika katika leza na vifaa vya kijeshi.

Urusi pia imekuwa na nia ya kuvutia wawekezaji kusaidia kuendeleza eneo lake la Arctic, Dmitriev alisema wiki iliyopita. Putin anataka biashara kuimarishwa kupitia Njia ya Bahari ya Kaskazini kupitia maji ya Arctic huku Urusi ikibadilisha biashara kuelekea Asia na mbali na Ulaya kwa sababu ya vikwazo vya Magharibi.

Kuzingatia umuhimu wa kimkakati wa Arctic kwa madini, usafiri wa meli na usalama wa kimataifa umeongezeka kwa kasi kwa sababu ya kauli za mara kwa mara za Trump kwamba anataka kupata Greenland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *